Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Huruma, Mwenye Rehema
Kwa Mtukufu Ayatollah udhma Khamenei, Kiongozi wa Mambo ya Waislamu duniani — Mwenyezi Mungu aendeleze kivuli chake kitukufu — Amani iwe juu yenu. Taifa, wanazuoni na masheikh wa Afghanistan wanawasilisha kwa kwako yafuatayo:
Katika wakati huu ambapo jeshi la ukafiri, likiwa katika sura ya Marekani mla-dunia na Wazayuni wauaji wa watoto, linaonesha makucha na meno na linatishia; juu ya vitisho na hofu hizi, mioyo yetu inapata faraja kwa kuwa tunayo hakika kwamba fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu, uangalizi wa Imam Sahib az-Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yake tukufu), pamoja na uongozi wa hekima wa Mtukufu wako, vimeienea Iran.
(Hakika sisi hatujawapuuzia katika kuwaangalia wala hatujawasahau katika kukukumbukeni). (Ewe mwana wa Abdul-Muttalib) hatujawaacha wala hatujawasahau; katikati ya hofu na fitna, macho yetu yako juu yenu.
Taifa, wanazuoni na masheikh wa Afghanistan wanaamini kwamba nyinyi mmebeba bendera ya Abul-Fadh’l al-‘Abbas mikononi, mko katika njia ya Hussein; mna subira ya Hasan moyoni; mna heshima na utulivu wa Abdul-Muttalib katika matendo; mna uwezo wa uongozi wa Abu Talib katika hali ya ufukara; mna haiba ya Muhammad (s.a.w.w) katika nafsi yenu, na ujasiri wa Ali katika mapambano.
Wanazuoni na maulama wa Afghanistan wanasubiri kwa hamu amri yeyote ile, kutoka kwako katika njia ya jihadi na ma dhidi ya ukafiri na ukanaji wa mungu wa kimataifa wa Kizayuni na Kimarekani, iwe ndani ya nchi za Kiislamu au nje yake, itakayotolewa na Mtukufu wenu.
Kwa shauku kubwa, tunasubiri amri yenu, ewe Kiongozi wa Mambo ya Uislamu duniani, Naibu wa Kiongozi wa Wahamiaji duniani, Hujjat bin al-Hasan (Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yake tukufu).
Toeni amri, ili wawe kama ndege wa Ababil juu ya adui mchafu wa Kimarekani na Kizayuni, na wawe kama watumwa wa Abu Dharr wakijitoa mhanga mbele yenu kwa mfano wa Karbala; ili wachukue hatua moja katika kuharakisha faraja ya Mtukifu huyo, ambaye faraja yake ni faraja ya ulimwengu mzima wa binadamu, chini ya uongozi wa Naibu wake.
Mwisho, tunamuomba Mwenyezi Mungu awasalie Muhammad na Aali za Muhammad (s.a.w.w), wale watukufu, wema na safi, ambao Mwenyezi Mungu Amefanya haki zao kuwa ni wajibu juu ya wote, utiifu na uongozi wao kuwa ni faradhi kwa kila mmoja, na pia Amefanya utiifu kwa Waliyy al-Faqih mtawala kuwa ni wajibu kwa watu wote.
Taifa, Wanazuoni na Masheikh wa Afghanistan
Maoni yako